MUHTASARI
Mashindano hayo yalidhaminiwa na kampuni mbalimbali, zikiwemo ASAS na Mkwawa Group of Companies, pamoja na TFS.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bwn. Musa Kilakala, ameipongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kufanikisha mashindano ya magari ya Serengeti Rally of Tanzania 2026.
Mashindano hayo yalifanyika katika Shamba la Miti Morogoro kwa kuhusisha magari 23 ya mashindano, ambapo kati ya magari hayo, madereva 21 walifanikiwa kumaliza mashindano hayo.

Akizungumza katika hafla maalumu ya kilele cha mashindano, Bwn. Kilakala alisema mashindano hayo yamewapa wananchi wa Morogoro, Watanzania na wageni kutoka nchi jirani fursa ya kujiburudisha na kujifunza.
“Mafanikio ya mashindano haya yamechangiwa na uwepo wa eneo linalofaa kwa shughuli hii, jambo ambalo limefanikishwa kwa kiasi kikubwa na TFS katika kulisimamia,” alieleza.
Alichukua fursa hiyo kuwapongeza TFS kwa kazi nzuri ya kuhakikisha eneo la mashindano linakuwa katika mazingira yanayowezesha kufanyika kwa mbio hizo za magari.
Aidha, kwa mujibu wa taarifa ya waandaaji wa mashindano hayo, jumla ya magari 23 yalishiriki, lakini madereva mawili yalishindwa kufika mwisho kutokana na changamoto za kiufundi, huku madereva 21 wakifanikiwa kukamilisha mbio hizo.
Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, Dkt. Hamza Kateti, alikuwa miongoni mwa viongozi wa Taasisi hiyo waliohudhuria hafla ya kilele.
Mashindano hayo yalidhaminiwa na kampuni mbalimbali, zikiwemo ASAS na Mkwawa Group of Companies, pamoja na TFS.

Serengeti Rally of Tanzania imekuwa ikifanyika kila mwaka katika Shamba la Miti Morogoro, eneo linalosimamiwa na TFS.
