MUHTASARI
Yajipanga kuweka mbele maslahi ya wateja nchini , kuboresha zaidi huduma za kiganjani, kidigitali
Bank of Africa Tanzania imezindua rasmi Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026, ikisisitiza dhamira yake ya kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja na kuboresha utoaji wa huduma za kifedha kiganjani na kidigitali katika kuleta uvumbuzi wa haraka kwa wateja.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa wiki ya wateja , Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Bwn. Wasia Mushi alisema kwamba benki hiyo kupitia wiki hiyo ya wateja watatumia mwezi mzima kutembelea matawi na kuzungumza na wateja wao nchini nzima.
“Tumedhamiria kujikita zaidi kwenye kuboresha huduma zetu kwa wateja kuweza kutatua changamoto zao za kifedha na kupanua zaidi wigo wa huduma za kifedha kwenye simu za kiganjani na kidigitali ili kwenda kurahisisha shughuli za kifedha kwa wateja wetu,”
“Tutatumia wiki hii kujiimarisha zaidi kwenye kutoa huduma zetu kwa kuwasikiliza zaidi wateja na kama kauli mbiu yetu inavyosema ‘kwenda hatua ya ziada’ kwenye kutafuta masuluhisho ya wateja kwenye shughuli zao za kila siku,” alisema Mushi.

Bw Wasia Mushi aliongeza kwambawateja wanaendelea kuwa kiini cha shughuli za Benki hiyo na mkakati wake wa utoaji wa huduma bora zaidi nchini.
Alisema kwenda “The Extra Mile” (hatua zaidi) kunamaanisha kuzidi matarajio ya wateja, kuelewa mahitaji yao ya kifedha yanayobadilika na kuendelea kutafuta njia bunifu za kufanya huduma za kibenki kuwa rahisi, za kuaminika na zinazopatikana kwa urahisi kupitia benki hiyo.
Aliongeza kuwa, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kuboresha uzoefu wa wateja, Bank of Africa Tanzania imeboresha programu yake ya huduma za kibenki kwa simu, B-Mobile, huduma za kiganjani kwa kuanzisha vipengele vinavyolenga kufanya huduma za kila siku za kibenki kuwa rahisi zaidi, zenye uwazi na za kuaminika.
“Maboresho haya yanaakisi mkazo wetu wa kimkakati katika mageuzi ya kidijitali, urahisi kwa wateja, uwazi na uaminifu wa huduma za kifedha hapa nchini,” alisisitiza.
Mushi aliongeza kwamba kupitia wiki hiyo ya wateja benki hiyo itafanya ziara kwenye matawi yake 18 nchini nzima katika juhudi za kuboresha mahusiano yao na wateja wake nchini nzima.
“Lengo letu ni kufanya huduma za kila siku za kibenki kuwa rahisi na za kuaminika zaidi, huku tukiendelea kuboresha namna tunavyowahudumia wateja wetu,” alifafanua.
Mushi aliongeza kwamba Benki hiyo imepata mafanikio ya kupewa cheti cha ISO 22301:2019, ambacho ni kiwango kinachotambulika kimataifa katika mifumo ya usimamizi wa mwendelezo wa shughuli za biashara (Business Continuity Management Systems – BCMS).
Alisema kwamba cheti hicho kinaonesha dhamira ya Benki katika kuimarisha uwezo wake wa kuendelea kutoa huduma wakati wa changamoto za kiutendaji, kupunguza hatari za kukwama kwa shughuli za biashara na kuhakikisha mwendelezo wa huduma muhimu za kibenki.
Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo, Bi. Annarobert Mango, alisema kaulimbiu ya “Going the Extra Mile” inaoneshwa kupitia mwingiliano wa kila siku kati ya Benki na wateja wake.
Alifafanua kwamba, kwenda hatua ya ziada kunamaanisha kusikiliza kwa makini, kuelewa mahitaji ya wateja, kutoa msaada kwa wakati na kumheshimu kila mteja.
“Huduma bora haiishii katika kutatua changamoto; pia inahusisha kutambua mahitaji kabla hayajatokea, kuwasiliana kwa uwazi na kuhakikisha wateja wanajisikia kuthaminiwa katika safari yao yote ya kibenki,” alisema.
Alisisitiza pia umuhimu wa mrejesho kutoka kwa wateja katika kuboresha utoaji wa huduma, huku akiwahimiza wateja kushirikisha Benki uzoefu wao, changamoto na mapendekezo.
Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha wateja wa Rejareja, Bwn. Asupya Nalingigwa, alizungumzia mkazo wa Benki katika kujenga mahusiano ya kudumu na wateja wa rejareja kwa kutoa suluhisho za kifedha zinazokidhi mahitaji yao, zinazopatikana kwa urahisi na zinazowarahisishia maisha ya kila siku pamoja na kutimiza matarajio yao ya kifedha ya muda mrefu.
Alisema mkakati wa Benki katika huduma za rejareja hauishii katika kutoa bidhaa za kifedha, bali unalenga kuelewa safari binafsi za kifedha za wateja, kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha na kutoa mwongozo na msaada unaowawezesha wateja kufanya maamuzi sahihi ya kifedha.
Uzinduzi huo pia ulitoa fursa kwa mmoja wa wateja wa Benki hiyo kueleza uzoefu wake na kutoa pongezi kwa Bank of Africa Tanzania.
Hilary Pato , Meneja Mkazi wa OCP Africa Tanzania limited, alieleza kuthamini kwa dhati dhamira ya Benki ya kuendelea kuelewa na kuitikia mahitaji ya wateja, akisisitiza ubora wa huduma, weledi, mwitikio na uhusiano mzuri alioupata katika kipindi chote cha ushirikiano wake na Benki hiyo.
Aidha, aliipongeza Bank of Africa Tanzania kwa dhamira yake ya kuwaweka wateja mbele na kuendelea kuboresha huduma zake ili kuongeza urahisi, thamani na kuboresha kwa ujumla uzoefu wa wateja katika huduma za kibenki.
Ushuhuda huo ulionesha umuhimu wa kujenga mahusiano ya kweli na ya muda mrefu na wateja, pamoja na kuonesha matokeo chanya ya mkakati wa Benki unaomweka mteja katikati ya huduma zake.
Katika uzinduzi huo, Bank of Africa Tanzania pia iliwatambua wateja wake watatu wa kampuni kwa kuendelea kuiamini na kujenga uhusiano na Benki hiyo. Wateja hao walikabidhiwa vikombe na Mkurugenzi Mtendaji kama ishara ya kuthamini imani, uaminifu na ushirikiano wao wa muda mrefu na Bank of Africa Tanzania.

Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 itaendelea katika kipindi chote cha mwezi huu, ikiwa na shughuli mbalimbali zinazolenga kuwathamini wateja, kuwashirikisha wafanyakazi na kuimarisha utamaduni wa kutoa huduma bora katika Benki nzima.
Benki hiyo inapoadhimisha kaulimbiu ya mwaka huu, “The Extra Mile,” Bank of Africa Tanzania imesisitiza tena dhamira yake ya kuwasikiliza wateja, kuitikia mahitaji yao ya kifedha, kutumia ubunifu wa kidijitali na kuendelea kuboresha uzoefu wa wateja katika huduma za kibenki.
KUHUSU BANK OF AFRICA (TANZANIA) LIMITED
BANK OF AFRICA – TANZANIA ni benki binafsi ya kibiashara inayofanya shughuli zake nchini Tanzania, ikihudumia wateja wa kampuni, biashara ndogo na za kati (SMEs) pamoja na wateja binafsi. Benki hiyo ilianza shughuli zake nchini Tanzania mwezi Juni 2007 baada ya kununua Eurafrican Bank, ambayo ilikuwa ikifanya shughuli zake nchini tangu Septemba 1995.
BANK OF AFRICA – TANZANIA ni sehemu ya BANK OF AFRICA GROUP, ambayo ilianza shughuli zake nchini Mali mwaka 1982.
BANK OF AFRICA GROUP ni kundi la benki la kimataifa la Kiafrika linalofanya shughuli zake katika nchi 20 za Afrika, likiwa na masoko katika Afrika Magharibi, Afrika Mashariki na Afrika ya Kati, pamoja na ofisi za uwakilishi jijini Paris, Hispania, London nchini Uingereza na China.
Tangu mwaka 2010, BANK OF AFRICA imekuwa kampuni tanzu inayomilikiwa kwa hisa nyingi na BMCE Bank, kundi la tatu kwa ukubwa la benki nchini Morocco, lenye uwepo katika nchi 31 katika mabara manne.
Kwa sasa, BANK OF AFRICA – TANZANIA ina mtandao wa matawi 18 ya huduma za rejareja, yakiwemo matawi tisa jijini Dar es Salaam na matawi tisa yaliyopo mikoani katika miji ya Arusha, Mwanza, Zanzibar na miji mingine mikuu.
