Img 20260923 Wa0043

Kamati Ya Bunge Ya Ustawi Na Maendeleo Ya Jamii Yaipongeza Barrick Bulyanhulu Kuzingatia Kanuni Za Afya Na Usalama Mahali Pa Kazi

MUHTASARI


Mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu unafanikisha kwa vitendo sheria ya usalama mahali pa kazi kwa kutumia zaidi mashine, mitambo na teknolojia za kisasa (Automation System)  kwenye maeneo hatarishi chini ya ardhi kama vile upasuaji wa miamba, ulipuzi na uchorongaji wa miamba.


KAMATI ya Kudumu ya Bunge Ustawi na Maendeleo ya Jamii  imefanya ziara ya kikazi katika mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu na kupongeza jitihada zinazofanywa na mgodi kuzingatia kanuni za usalama mahali pa kazi,kujali afya za wafanyakazi wake na jamii nzima ya vijiji vinavyozunguka mgodi huo.

Pia kamati imepongeza uwekezaji mkubwa wa kampuni katika matumizi ya teknolojia za kisasa ambazo zimefanikisha kuwaweka wafanyakazi wake katika mazingira mazuri zaidi ya kufanyia kazi ambayo si hatarishi ya kusababisha matukio ya ajali na kuathiri afya za wafanyakazi wake.

Mwenyekiti wa kudumu wa kamati hiyo, Bi. Hawa Mchafu Chakoma,  akiongea baada ya kuhitimisha ziara hiyo amesema Kamati imeridhishwa kwa jinsi mgodi unavyotekeleza sheria za kazi , programu za afya na usalama mahali pa kazi.

“Tunawapongeza kwa  kuwa kinara wa masuala ya usalama mahali pa kazi ambapo mwaka huu mmeshinda tuzo  mbalimbali za OSHA.Vilevile Katika wasilisho lenu tumeona ni jinsi gani kampuni ya Barrick iko mstari wa mbele kulinda afya za wafanyakazi wake na jamii nzima ya maeneo yanayozunguka mgodi na kwa jinsi inavyofanikisha miradi ya Afya kupitia fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) pia tumefurahi kusikia inavyotekeleza kwa vitendo sheria ya ushirikishwaji watanzania katika mnyororo wa thamani kwenye sekta ya madini (Maudhui ya Ndani ),”alisema Mh.Chakoma.

Kwa niaba ya Kamati, Mh.Chakoma ametoa mapendekezo kuwa mgodi uhakikishe elimu ya Afya na Usalama inawafikia pia wafanyakazi wote na wakandarasi wote wanaofanya kazio na mgodi.


“Ni kweli kwenye wasilisho lenu  tumeona hakuna kifo au ajali kubwa hata moja tangu mwaka huu uanze nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa kazi kubwa ila muhimu kwa wafanyakazi wote kupata mafunzo na kujengewa uwezo wa usalama na afya kwenye maeneo yao ya kazi,” aliongeza Mwenyekiti huyo wa Kamati hiyo ya maendeleo ya ustawi wa Jamii.

Chakoma alisema kwamba mazingira mazuri ya kazi yanaongeza tija kwenye uzalishaji na kutengeneza wigo mpana zaidi kwa serikali kufanya kazi kwa pamoja na wawekezaji wa ndani na nje kwenye sekta ya madini nchini.

Img 20260923 Wa0045
 Mwenyekiti wa Kudumu wa Kamati ya Bunge Ustawi na Maendeleo ya Jamii , Hawa Mchafu Chakoma akizungumza kwenye ziara hiyo , katikati ni  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi , Ajira na Mahusiano , Dkt Evaline Munisi na wa kwanza kushoto ni Meneja Mkuu wa Barrick Bulyanhulu , Rhys Harvey.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu kazi , Ajira na Mahusiano, Dkt Evaline Munisi ameupongeza Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kuwa kinara wa utekelezaji wa sheria za kazi, ajira , usalama na afya mahali pa kazi na umefanyiwa ukaguzi mwanzoni mwa mwaka huu na kukidhi viwango vya Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa kazi (OSHA) na kupatiwa Ithibati hali iliyopelekea mgodi ushinde tuzo saba za OSHA.

Aliongeza kuwa mgodi unatekeleza kwa viwango vya juu sheria za kazi, usalama na afaya mahali pa kazi ya sura 297 na umekidhi matakwa ya sheria hizo pamoja na wakandarasi  wanaofanya kazi na mgodi huo.

Dkt Munisi alisema wizara hiyo kwa kushirikiana na OSHA imefanya kaguzi mbalimbali ambapo katika kipindi cha mwaka 2025/26 jumla ya kaguzi 871 zilifanyika na wafanyakazi 7,969 walipimwa afya zao katika Mkoa wa Shinyanga na waajiri 102 walikuwa wametekeleza sheria ya usalama na afya na kupatiwa leseni ya ithibati.

Awali akitoa taarifa kwa Kamati hiyo, Meneja Mahusiano ya Jamii na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu , Agapiti Paul alisema mgodi huo unafanikisha kwa vitendo sheria ya usalama mahali pa kazi kwa kutumia zaidi mashine, mitambo na teknolojia za kisasa (automation system)  kwenye maeneo hatarishi chini ardhi kama vile upasuaji wa miamba , ulipuzi na uchorongaji wa miamba.

“Moja ya sera ya kampuni ya Barrick Bulyanhulu ni kuweka mbele afya ya wafanyakazi wake na tuna kauli mbiu kwamba unakuja kazini na  kurudi nyumbani salama,” alisema Paul

Paul ameongeza kuwa mbali na kuimarisha huduma za afya na usalama ndani ya mgodi pia umekuwa mstari wa mbele kuboresha kituo cha afya cha Bugarama na kupeleka kampeni ya kupambana na Malaria ijulikanayo kama ‘Zero Malaria’ kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi kwa kupuliza dawa za kuua mazalia ya mbu na kuwagawia wananchi vyandarua vyenye dawa.

Aliongeza kwamba mgodi huo kupitia sera na kanuni ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kila mwaka unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali kwenye maeneo ya afya , barabara , ujenzi wa mashule , mabweni na kilimo kwa kuwajengea uwezo vijana hasa wanaozunguka mgodi kupata shughuli za kujiingiza kipato,” alisema

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bwn Frank Nkinda alishukuru Barrick Bulyanhulu kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo na kushirikiana na vijiji 16 vinavyozunguka mgodi huo kwa kuwapatia wanawake , vijana na makundi mbalimbali katika jamii nafasi ya kufanya kazi na mgodi huo ili kujikwamua kwenye umasikini wa kipato sambamba na uwekezaji wake kufanikisha miradi mikubwa ya maendeleo.

Img 20260922 Wa0044 Previous post Tanzania Sasa Mwenyekiti Mwenza Katika Jukwaa la Mawaziri Beijin
Img F8b631c5 2120 4794 8012 85b575263e22 Next post Wakulima 8,000 Kunufaika Na Awamu Ya Pili Ya Utekelezaji Wa Mradi Wa Kilimo Thabiti