E181cab1 3bdb 4743 Aa88 436ad0ab50af 780x470 1

UZINDUZI WA JNHPP: Tanzania Kuandika Historia Mpya Kwenye Uzalishaji Umeme

 

MUHTASARI


Uwezo wa Tanzania wa kuzalisha umeme umefikia megawati 4,446 dhidi ya mahitaji ya juu ya gridi ya taifa hali ambayo imeiwezesha nchi kuanza kutumia ziada hiyo kwa ajili ya biashara ya umeme.


PWANI: WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema uzinduzi wa mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) ni hatua muhimu katika kuongeza uwezo wa Tanzania kuzalisha umeme na kuifanya nchi kuwa kitovu cha biashara ya nishati katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Ndejembi amesema kituo hicho kina mitambo tisa, ambapo kila mtambo una uwezo wa kuzalisha megawati 235, na kufanya uwezo wa jumla kufikia megawati 2,115.

Amesema ongezeko hilo limeimarisha uwezo wa taifa kukidhi mahitaji ya umeme kwa shughuli za uzalishaji, uwekezaji na ukuaji wa uchumi, huku likiiweka Tanzania katika nafasi muhimu ya kuunganisha masoko ya umeme ya kikanda.

“Tanzania ni mwanachama wa East African Power Pool na Southern Africa Power Pool, ambapo nchi yetu inaunganisha mtandao wa umeme kikanda,” amesema Ndejembi.

Kwa mujibu wa Ndejembi, uwezo wa Tanzania wa kuzalisha umeme umefikia megawati 4,446 dhidi ya mahitaji ya juu ya gridi ya taifa hali ambayo imeiwezesha nchi kuanza kutumia ziada hiyo kwa ajili ya biashara ya umeme.

Amesema Tanzania tayari imeingia makubaliano na Zambia kwa ajili ya kuiuzia umeme, huku ikiwa pia na makubaliano na Kenya ya kuuziana umeme kulingana na mahitaji ya kila nchi.

Ndejembi ameongeza kuwa Serikali inaendelea na mazungumzo na nchi nyingine jirani ili kuuza au kununua umeme pale unapohitajika.

Img 20260808 Wa0008 Previous post Ripoti ya LHRC ya mazingira ,Mabadiliko ya Tabia Nchi na Watetezi Haki za Mazingira Yaibua “Mazito”
O0a06411 Next post Mhandisi Innocent Masaka: Mtaalamu Kijana Wa Kilimo Aliyebeba Maono Ya Kuipa ASA Muelekeo Mpya