Img 20260926 Wa0004

NHIF, Hospitali Ya Aga Khan Zaingia Makubaliano Matibabu Ya Wagonjwa Wa Saratani 

MUHTASARI


Wanachama wa NHIF sasa wanaweza kupata tiba ya magonjwa ya saratani katika Hospitali za Aga Khan Dar es Salaam, Mwanza, na kwenye Kiliniki 14


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umesaini makubaliano na Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam yatakayowawezesha wanachama wake kupata huduma za matibabu ya saratani, ikiwamo tiba kwa mionzi na kemikali.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dk. Irene C. Isaka, pamoja na Mtendaji Mkuu wa Aga Khan Kanda ya Afrika Mashariki, Dk. Zeenat Sulaiman, jijini Dar es Salaam.

Img 20260926 Wa0011
 

Dk. Irene amesema   yanalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kibingwa kwa wanachama wa NHIF kupitia Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam, Mwanza na kliniki 14.

Amesema  ushirikiano huo ni sehemu ya jitihada za Mfuko kupanua wigo wa huduma za afya na kuboresha upatikanaji wa matibabu ya kibingwa kwa wanachama wake.

Amesema makubaliano hayo yanaendeleza ushirikiano wa muda mrefu kati ya taasisi hizo na kuimarisha upatikanaji wa huduma za saratani wakati Serikali ikiendelea kutekeleza mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.

Dk. Zeenat  amesema ushirikiano huo unaimarisha dhamira ya taasisi hizo katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Amesema Hospitali ya Aga Khan itaendelea kutumia utaalamu, teknolojia na uzoefu wake kutoa huduma za matibabu ya saratani kwa kuzingatia viwango vya  vya kisasa.

Img 20260924 Wa0085 Previous post Wakala Wa Misitu Tanzania Yataka Watumishi Kuimarisha Uadilifu, Usimamizi Wa Vihatarishi
Img 20260927 Wa0007 Next post Taifa Gas Yaendelea Kufanikisha Mkakati Wa Kitaifa Wa Matumizi Ya Nishati Safi