Img 20260826 Wa0002

Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar Chabuni Teknolojia Za Kuwasaidia Wavuvi na Wachimbaji Madini Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Tanga

MUHTASARI


Teknolojia hiyo inalenga kuwawezesha wavuvi kupata masoko yenye tija kwa mazao yao, kuongeza kipato na kutumia fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi.


Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimekuja na teknolojia na tafiti mbalimbali zinazolenga kuwasaidia wavuvi na wachimbaji wadogo wa madini,  ili kuweza kupata tija pamoja na  kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za uzalishaji.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho , Prof. Said Ali Hamad Vuai, amesema chuo hicho kinafanya utafiti wa soko la kimtandao kwa mazao ya uvuvi, unaolenga kuwaunganisha wavuvi na wanunuzi ndani na nje ya Tanzania.

Amesema teknolojia hiyo inalenga kuwawezesha wavuvi kupata masoko yenye tija kwa mazao yao, kuongeza kipato na kutumia fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi.

Img 20260826 Wa0003 1

Aidha, ameongeza kuwa tafiti hizo ni sehemu ya juhudi za SUZA kutumia elimu, teknolojia na ubunifu kutatua changamoto halisi zinazowakabili wananchi na kuchochea maendeleo ya Taifa.

“Tunataka elimu na tafiti tunazofanya ziwe na manufaa kwa jamii, zisaidie kutatua changamoto na kuongeza thamani katika shughuli za uzalishaji”.

Ameeleza kuwa mbali na tafiti na ubunifu, SUZA inatoa programu mbalimbali za elimu kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada na viwango vya juu vya kitaaluma katika maeneo ya teknolojia, afya, famasia, sayansi, kilimo, ufugaji, biashara, ujasiriamali, masoko, ununuzi na ugavi, elimu pamoja na uandishi wa habari.

Prof. Vuai amewataka wananchi wanaoshiriki Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kutembelea banda la SUZA ili kufahamu zaidi kuhusu teknolojia, tafiti na programu za elimu zinazotolewa na chuo hicho.

Amesema SUZA inaendelea kutoa fursa kwa vijana kutoka Tanzania na nje ya nchi kutumia elimu na ubunifu kama nyenzo ya kutatua changamoto za jamii na kujenga fursa za kiuchumi.

Naye Mudrick Mohamed Iddi kutoka SUZA, amebuni teknolojia ya kuwasaidia wachimbaji madini kupeleka taarifa juu yeye awepo chini ya ardhi endapo atakumbwa na changamoto yoyote bila kutumia simu hivyo kutumia Mesh Network.

Img 20260824 Wa0015 Previous post Msaada Wa TFS Wa Madawati Yenye Thamani Ya Sh Milioni 7 Waweka Tabasamu Kwa Wanafunzi Ifakara
Img 20260830 Wa0002 Next post Nidhamu, Uadilifu na Mnyororo wa Amri : Msingi wa Jeshi Imara la Uhifadhi Tanzania